Klabu ya KCCA FC Under 20 ya nchini Uganda imejinyakulia ubingwa siku ya Jana katika michuano ya fainali za michuano ya Cambiasso U-20 International Tournament 2022 dhidi ya klabu ya Azam FC iliyochezwa katika kiwanja cha CHAMAZI COMPLEX kwa ushindi wa goli 1-0 hivyo kuandika historia ya kuwa klabu ya kwanza kushinda taji hilo likiwa ndio kwanza limeanzishwa.