
Ikiwa bado zimesalia siku kadhaa kuelekea michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara kampuni ya michezo ya kubashiri, M-Bet ikiwa ni mdhamiani mkuu wa klabu YA Simba SC yaja na mkataba mnono kwa ajili ya klabu hio ambao utadumu kwa muda wa miaka 5. “M-Bet ni kampuni namba moja ya michezo ya kubashiri sasa tunashirikiana na klabu namba moja Tanzania.”
“Tunaamini kama M-Bet tukishirikiana na Simba tutajitangaza ndani na nje ya Tanzania.”
“Mwaka wa kwanza – Bil 4.670
Mwaka wa pili – Bil 4.925
Mwaka wa tatu – Bil 5.205
Mwaka wa nne – Bil 5.514
Mwaka wa tano – Bil 5.853
Jumla ni Bilioni 26, milioni 168 na Tsh. 5,000.”- Mkurugenzi wa Masoko wa M-Bet, Allen Mushi.