
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan amewaagiza wateule wake katika Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji mapato na kudhibiti matumishi huku akiitaka Ofisi ya Rais-TAMISEMI kufanya mapitio ya viwango vilivyowekwa.
Rais Samia ametoa kauli hiyo mara baada ya kuwaapisha wakuu wa Mikoa na makatibu Tawala wa Mikoa aliowateua hivi karibuni
” TAMISEMI ndio watumiaji wa kubwa wa fedha lakini makusanyo ni kidogo sana. Niwapongeze kwa kuvuka lengo katika ukusanyaji wa mwaka 2021/22 Kwa kukusanya Kwa asilimia 103, lakini kuna haja ya kufanya mapitio ya viwango vya ukusanyajia mlivyoviweka nina hakika mnaweza kukusanya zaidi.
” Viwango vimewekwa kwa mazoea lakini tukipanga viwango vikubwa na fedha zitakusanyika kama kweli tutakwenda kukusanya na kuziba mianya, mapato yakikusanywa mambo madogo madogo mnayoyataka mtaweza kuyatekeleza.”
Rais Samia alitolea mfano mabadiliko ya uongozi aliyoyafanya kayika Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro aliyoongeza ukusanyaji mapato hayua ambayo imefanya wachangie ujenzi wa hospitali ya Wilaya na kiwataka kuinga mfano huo.
” Sina mswalie Mtume na mapato na matumizi, fedha nyingi tunazileta kwenye Mikoa na Wilaya kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
Kuna kipindi nilizungumza anayetaka kujua rangi yangu achezee hizo fedha, lakini wakajitokeza wanaume wakataka kujaribu wameiona rangi halisi nasema tena na leo kunafedha nyingi zinashuka huko na haziletwi ili mcheze bali kwa ajili ya kusukuma miradi ya maendeleo kwa ajili ya wananchi.
Amesema kama kuna haja ya kubadilisha matumizi ya fedha zilizopelekwa ni lazima zifanyike taratibu zinazotakiwa na maamuzi yafanye na baraza madiwani na kuwataka kuacha mvutano.