Ikiwa zimesalia siku kadhaa kuelekea maadhimisho maalumu ya Simba Day, Klabu ya Simba SC nchini Tanzania imejiandaa vema kwenda kutembelea nyumba ya wazee Kigamboni leo hii ili kuweza kuwapa faraja nao wajihisi wako pamoja nao ni suala la muda tu kuwaweka kando. Kupitia kurasa zao za mitandao klabu hiyo imeweka hayo bayana kama ifuatavyo.
“Leo saa 6:00 mchana tutakuwepo kwenye Nyumba ya Wazee Kigamboni ili kuwapa faraja wazee wetu na kutoa zawadi ambayo tumepanga kuwakabidhi. Wanasimba wote mnakaribishwa.
Zoezi hili la kurudisha kwa jamii linafanyika katika mikoa yote Tanzania”.