Manchester United wanatazamia kuwauza mabeki sita kabla ya dirisha la usajili kukamilika mwezi huu (Mail)
Leicester City wameiambia Newcastle United kwamba watahitaji kulipa pauni milioni 60 ikiwa watamsajili kiungo wa kati wa Uingereza James Maddison, 25. (Football Insider)
Kipa na nahodha wa Leicester Kasper Schmeichel, 35, anakaribia kujiunga na Nice ya Ufaransa na atafanyiwa vipimo vya afya wiki hii, na hivyo kuhitimisha miaka 11 ya kukaa na Foxes.. (Mail)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
RB Leipzig wanaongoza katika kinyang’anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na Ujerumani Timo Werner, 26, mbele ya Juventus.
Klabu hiyo ya Stamford Bridge ina beki wa Leipzig na Croatia Josko Gvardiol, 20, juu ya orodha yao ya uhamisho na wanaweza kuomba makubaliano ya kubadilishana. (Fabrizio Romano)
Red Bull Salzburg wako tayari kutoa ofa zaidi ya £45m kwa fowadi wa Slovenia Benjamin Sesko, 19, ambaye analengwa na Manchester United, Chelsea na Newcastle. (i Sport)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Chelsea wamezuia uhamisho wa Fulham kumnunua beki Mfaransa Malang Sarr, 23. The Cottagers pia wamewasilisha ombi la kumnunua beki wa kati wa West Ham Mfaransa Issa Diop, 25. (Standard)
Napoli wapo kwenye mazungumzo na Chelsea kuhusu kumsajili kwa mkopo kipa wa Uhispania Kepa Arrizabalaga, 27.. (Sky Sports)
Chelsea wanakaribia kukamilisha usajili wa mlinda mlango Mmarekani Gabriel Slonina, 18, kutoka Chicago Fire, ambapo atasalia kwa mkopo hadi Januari. (Fabrizio Romano)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Mshambulizi wa Chelsea na Ubelgiji Michy Batshuayi, 28, yuko tayari kuhamia Everton msimu huu wa joto. (Talksport)
Beki wa United na Ivory Coast Eric Bailly, 28, amekataa kuungana tena na Jose Mourinho katika klabu ya Roma akipendelea kuhamia Sevilla.. (Sun)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Mlinda mlango wa Arsenal na Ujerumani Bernd Leno, 30, anatazamiwa kujiunga na Fulham baada ya vilabu hivyo kukubaliana juu ya mkataba wa £8m na masharti ya kibinafsi kutatuliwa. (Guardian)
Fulham na Bournemouth wanataka kumsajili beki wa kati wa Liverpool Nat Phillips, 25, lakini Reds wanataka zaidi ya £10m kwa Muingereza huyo. (Goal)
Mshambulizi wa Arsenal Folarin Balogun, 21, anakaribia kujiunga na klabu ya Ufaransa ya Reims kwa mkataba wa mkopo wa msimu mzima. (Mail)
Mshambulizi wa zamani wa Manchester United na Arsenal Alexis Sanchez amekatiza kandarasi yake ya Inter Milan na kuwa mchezaji huru, huku Marseille wakitaka kumsajili mchezaji huyo wa Chile mwenye umri wa miaka 33.. (Sky Sports)
Source: BBC SWAHILI