Benki ya NBC imeendelea kung’ara kwenye Maonesho ya Kilimo Nanenane yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya, huku huduma ya Bima ya Kilimo inayotolewa kupitia Benki ya NBC kwa wakulima ikiwa ni moja ya vivutio vikubwa miongoni mwa washiriki wanaotembelea maonesho hayo.
Akizungumza kwenye maonesho hayo yaliyozinduliwa juzi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango, Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo, Lariba na wakulima kutoka Benki ya NBC, Bw. Raymond Urassa alisema ushiriki wa Benki ya NBC kwenye maonesho haya ni muendelezo wa jitihada zetu za kuendelea kujiweka karibu zaidi na wadau wa sekta hii muhimu.