Benki ya CRDB Plc nchini Tanzania ikiwa ni moja ya wadau katika Sekta ya kukuza uchumi imeeleza kwamba imeshiriki katika kongamano la nne (4) la wadau wa sekta ya Nishati Tanzania, ndani na nje ya Afrika. Ikiwa mwaka huu Kongamano limeangazia masuala muhimu katika sekta ya nishati nchini Tanzania yanayohusu bomba la EACOP (East Africa Crude Oil Pipeline) maendeleo ya gesi ya baharini, mazungumzo ya mradi wa LNG (Tanzania Liquidified Natural Gas) na mapendekezo kadhaa ya mradi wa nishati mbadala. Tanzania imeendelea kuwezesha kwa ufanisi fursa mpya za kibiashara kwa upande wa nishati katika Afrika Mashariki ambapo, benki yetu ya CRDB ikiwa ni mdau mkubwa wa maendeleo na uchumi imeshiriki katika kuihakikishia serikali na wadau wote wa sekta binafsi utayari wetu katika kuwahudumia wateja kwa kuwaongezea mitaji katika utekelezaji wa miradi kupitia huduma zetu za asset financing, overdraft, na invoice discounting
Nmb Yashiriki Kilele Cha Wiki Ya Sheria Dodoma
Benki ya NMB imeshiriki kilele cha wiki ya Sheria nchini iliyomalizika leo jijini Dodoma. Pichani, Meneja wa Kanda...
Read more