Benki ya Taifa ya Biashara NBC imetoa milioni 10 kwaajili ya mashindano ya mchezo wa Golf yafahamikayo kama NBC Lugalo Patron Trophy 2022 yatakayofanyika Agosti 27 mwaka huu yakijumuisha Division A,B na C Juniors, Ladies na Seniors. Shindano hili litajumuhisha wachezaji kutoka klabu zote za hapa nchini kama vile Moshi Club,Arusha Gymkhana, Mufindi Club, Morogoro Gymkhana, Dar es Salaam Gymkhana, Sea Cliff Golf Club Zanzibar, Kili Golf na TPC Golf Club. Yameandaliwa ili kumuaga Jenerali Venance Mabeyo na kumkaribisha Mlezi mpya wa Klabu ya Golf Jenerali Jacob Mkunda. Mgeni rasmi katika mashindano hayo anategemewa kuwa mheshimiwa Waziri mwenye dhamana ya michezo Mohamed Mchengerwa.
Mwili wa Memes, Aliyekufa Vitani Ukraine Wawasili Tanzania
Ndugu na jamaa wa Mtanzania Nemes Tarimo wameupokea mwili wa kijana huyo leo alfajiri katika uwanja wa ndege wa Jijini...
Read more