
Leo hii Benki ya CRDB imeungana na wateja wake wa Kanda ya Ziwa (Lake Zone) kusherekea ushindi wa tuzo ya Euromoney waliyoshinda hivi karibuni nchini Uingereza. Hafla hii fupi ya kutoa shukrani kwa wateja wao wa Kanda ya ziwa ilifanyika katika tawi la CRDB Bank Rock City.
Benki inajivunia mafanikio hayo, na kuwashukuru wateja, wanahisa wao, Serikali, na washirika wao wote kwa kuwa sehemu ya safari ya mafanikio hayo.
Ahadi yao ni kuendeleza ubunifu katika huduma zao, na kushirikiana na wadau wao ikiwemo Serikali ili kuboresha maisha ya Watanzania na uchumi wa Taifa letu.


