Klabu ya Simba SC kupitia maadhimisho ya Tamasha lao maalumu linalofanyika kila mwaka kabla ya msimu mpya wa Ligi kuu kuanza, Simba Day imewatambulisha wachezaji wapya na waliosalia kikosini hapo kuhudumu kwa msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023.