
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma TCRA, Bi. Lucy Mbogoro akizungumza na wananchi wa mkoa wa Mbeya na mikoa jirani waliofika katika banda la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) siku ya Kilele cha Maonesho ya Kilimo- NaneNane kitaifa yaliyofanyika katika viwanja vya John Mwakangale,Uyole jijini Mbeya tarehe 8 Agosti, 2022.
TCRA imeshiriki #nanenane2022 2022 kuwasilisha ujumbe wa kampeni ya elimu kwa umma iitwayo “Kwea Kidijitali” inayosisitiza matumizi salama na sahihi ya Mawasiliano katika kukuza Uchumi wa Kidijitali
Kauli Mbiu: “Kilimo ni Biashara, Shiriki Kuhesabiwa kwa Mipango Bora ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi.”



