
Mwonekano wa Soko kuu la Kisasa la Njombe Mji lenye ukubwa wa mita za mraba 9,186 lina sakafu (floors) 3. Soko lina mifumo na sehemu mbalimbali yakiwemo; Maduka 162, Meza za biashara 407, Vyoo 47, Migahawa 2, Stoo 6, vizimba vya Kuku 27, Machinjio ya wanyama wadogo, Sehemu za huduma za kibenki 2, ofisi za utawala 2, Mfumo wa maji safi na maji taka, kisima kirefu cha maji.
Pia, Soko lina Tanki la maji la ardhini lenye ujazo wa lita 500,000 pamoja na pampu ya kupandisha maji, Mfumo wa kutambua
viashiria vya majanga ya moto (fire detector system), Mfumo wa kupambana na majanga ya moto (Fire fighting system), Mfumo wa kamera za kiusalama (CCTV Camera system); Mfumo wa habari na mawasiliano (Data and Voice system/PA System) na sehemu za maengesho ya magari yapatayo 120 kwa wakati mmoja.
Aidha kwa mujibu wa michoro ya usanifu soko lilipangwa kuhudumia wafanyabiashara wasiopungua 630 na limeghalimu thamani ya shilingi Bilioni 10.2


source: OR-TAMISEMI