ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 12.08.2022

Barani Ulaya

ADVERTISEMENT

Marcus Rashford

Paris St-Germain wako kwenye mazungumzo na wawakilishi wa Marcus Rashford kuhusu uwezekano wa kumsajili mshambuliaji huyo wa Uingereza, 24, kutoka Manchester United. (L’Equipe – kwa Kifaransa)

United pia wana mkutano ulioratibiwa na mamake Adrien Rabiot na wakala wake baada ya kukubaliana ada na Juventus kumnunua kiungo wa kati wa Ufaransa, 27. (Fabrizio Romano).

Manchester City wana nia ya kumsajili beki wa kushoto wa Atletico Madrid wa Brazil Renan Lodi, 24. (Telegraph – usajili unahitajika)

Pia unaweza kusoma:

Beki wa kushoto wa Arsenal Kieran Tierney, 25, pia ni miongoni mwa majina kwenye orodha ya wanaowania Manchester City. (90 Minutes)

Mshambulizi wa zamani wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 33, angependelea kusalia Barcelona kuliko kurejea katika Ligi ya Premia akiwa na Chelsea. (Sport, via Metro)

Nottingham Forest wamewasilisha ombi la kwanza kwa mshambuliaji wa Watford na Nigeria Emmanuel Dennis, 24. (The Athletic).

gett

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Beki wa kushoto wa Arsenal Kieran Tierney ananyatiwa na Man City

Atalanta itachuana na Forest katika kumsajili winga wa Italia Emerson Palmieri, 28, kutoka Chelsea. (Standard)

Everton wanatarajia kukamilisha dili la kumsajili mshambuliaji wa Guinea Serhou Guirassy, ​​26, kutoka Rennes kabla ya mwisho wa juma. (L’Equipe – kwa Kifaransa)

Che Adams wa Southampton ana nia ya kutaka kuhamia Everton, lakini kuna ushindani kutoka kwa Leeds United, Wolves na Forest kwa mshambuliaji huyo wa Scotland, 26. (Mail).

Che Adams

CHANZO CHA PICHA,SNS

Maelezo ya picha,Che Adams wa Southampton

Aliyekuwa mkufunzi wa muda wa Manchester United Ralf Rangnick amependekeza kwamba mshambuliaji wa Stuttgart na Austria Sasa Kalajdzic, 25, anapaswa kukataa kuhamia Old Trafford. (Star)

Juventus wanakaribia kukamilisha dili la kumnunua mshambuiaji wa Barcelona na Uholanzi Memphis Depay, 28. (90min).

Marseille wamefanya mawasiliano na Manchester United kuhusu mkataba wa mkopo wa beki wa Ivory Coast Eric Bailly, 28. (L’Equipe – in French)

beki wa Ivory Coast Eric Bailly

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Beki wa Ivory Coast Eric Bailly

Winga wa Bayer Leverkusen Mhispania Iker Bravo, 17, atajiunga na Real Madrid kwa mkopo wa msimu mzima. (Bild – kwa Kijerumani)

Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea na Uhispania Diego Costa, 33, anarejea Rayo Vallecano baada ya kutokuwa na klabu tangu kandarasi yake ya Atletico Mineiro ilipomalizika mwezi Januari. (Marca)

CHANZO: BBC SWAHILI

ADVERTISEMENT

RelatedPosts

Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ADVERTISEMENT

Welcome Back!

Login to your account below

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.