
Benki ya Taifa ya Biashara, NBC imesisitiza kuhusu adhma yake ya kukuza na kuendeleza sekta ya michezo hapa nchini kwa kuunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali pamoja na wadau wengine wa sekta ya michezo inayokua kwa kasi.
Akizungumza kwenye hafla ya jioni iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam ikilenga kuwapongeza na kuwakaribisha wanamichezo wa Kitanzania walioshiriki kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika hivi karibuni Birmingham, Uingereza, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw. Theobald Sabi alisema sekta ya michezo, sanaa na utamaduni ina mchango muhimu katika suala zima la ajira pamoja na kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja na pato la taifa kwa ujumla.



NBC Tanzania
Financial Service