Mchezaji mahiri wa soka nchini Tanzania aliyekuwa anakipiga katika klabu ya Coastal Union FC, ambaye kwa sasa amesaini kuitumikia klabu ya Azam FC Abdul Suleiman Sopu amekabidhiwa zawadi ya kuku na shabiki wa klabu anayeitumikia kwa sasa kwa sababu ya kufunga Hat-trick katika michuano ya fainali ya Kombe la Shirikisho la AZAM SPORTS akiwa bado katika klabu yake ya zamani Coastal Union FC dhidi ya Klabu ya Yanga kwenye mchezo uliochezwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abed jijini Arusha ikiwa ni namna ya kumpongeza mchezaji huyo kwa jitihada anazozionyesha katika Soka Tanzania Bara.