
Kampuni ya Mawasiliano Halotel ikiongozwa na Naibu Mkurugenzi Bwana Minh Xuan Dong (wa pili kushoto) na Naibu Mkurugenzi wa huduma ya Halopesa Bwana Magesa Wandwi (wa kwanza kulia, wamemtembelea Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali wa Polisi, Camilius Wambura katika ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Jijini Dar es Salaam.
Katika Mazungumzo yao, Naibu Mkurugenzi huyo alitumia fursa hiyo kumpongeza Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Wambura kwa kuteuliwa kuwa Mkuu Mpya wa Jeshi la Polisi nchini, na kumuahidi kuendeleza ushirikiano baina ya Jeshi la Polisi na Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel. #Halotel

