
Ikiwa ni miongoni mwa jitihada za kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamuhuri ya Muuungano wa Tanzania kuhusu masuala ya SENSA 2022,Mkurugenzi mtedaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela na Timu yake waKIungana na Wadau kutokea Wizara yenye dhamana ya Tamaduni, Sanaa na Michezo ili kuhamasisha watu kuweza kujitokeza kwa wingi katika zoezi zima la Sensa ili waweze kuhesabiwa #SENSABIKA
Kutokea kuraza za mitandao ya kijamii Benki ya CRDB “
leo tumeungana na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo pamoja na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) katika kuadhimisha siku ya kilele cha Tamasha la kuhamasisha wananchi kuhesabiwa kwenye Sensa 2022 linalofahamika kama #SensaBika.
Tamasha hilo linalofanyika katika viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar es salaam na kuhusisha shughuli mbalimbali za kisanii na michezo”.







