Matokeo ya mechi za Ligi kuu ya NBC Tanzania Bara zilizochezwa Agosti 21, 2022 yapo kama ifuatavyo; Mechi kati ya Mtibwa Sugar FC na Ruvu Shooting FC 2-1 iliyochezwa uwanja wa Manungu, Polisi Tanzania FC na KMC 2-2 iliyochezwa uwanja wa Sheik Amri Abeid, Singida Big Stars FC na Mbeya City FC 2-1 imechezwa uwanja wa Liti, na Azam FC vs Geita Gold FC 1-1 imechezwa uwanja wa Azam Compex Chamazi.