Benki ya NMB imetoa kiasi cha Tsh. 20,000,000/- katika chuo cha kitaifa cha utalii Ili kuhakikisha sekta ya utalii inaendelea kukua nchini, imeshiriki na kudhamini programu ya mafunzo kwa wadau zaidi ya 5000 walio katika mnyororo wa thamani wa sekta hio, kwa lengo la kuimarisha huduma, na kukuza maendeleo ya nchi.
Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo alikuwa Waziri wa Maliasili na Utalii – Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana , Afisa Mtendaji Mkuu Chuo Cha Taifa Cha Utalii- Dkt. Shogo Mlozi, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji – Dkt. Anna Makakala na wamewakilishwa na Afisa Mkuu wao wa Rasilimali Watu- Ndg. Emmanuel Akonaay.