Winga wa Ajax Mbrazil Antony, 22, anashinikiza kujiunga na Manchester United kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili msimu huu. (Goal)
Hata hivyo, United wanasalia katika kumwinda winga wa PSV Eindhoven Mholanzi Cody Gakpo, 23 lakini wana uwezekano wa kusajili mmoja wa washambuliaji kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Telegraph)
United pia wanajiandaa kushinikiza kwa mara ya mwisho mwezi huu kumsajili kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong, 25. (Marcel van der Kraan, via Express)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Klabu hiyo ya Old Trafford itazuia uhamisho wowote wa mlinzi wa Uingereza Harry Maguire baada ya Chelsea kumuulizia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29. (Sun)
AC Milan wametumia mbinu nyingine kumnunua beki wa kati wa Tottenham Muingereza Japhet Tanganga, 23. (Calciomercato – in Italian)
Newcastle wanatumai kupata uhamisho wiki hii huku klabu hiyo ikifanyia kazi mikataba miwili na kuamini uhamisho wa mshambuliaji wa Watford raia wa Brazil. Joao Pedro, 20, inawezekana. (iNews)
Kiungo wa kati wa Manchester City na Uingereza Keira Walsh, 25, bado anawindwa na Barcelona. (Sport – in Spanish)

Nice wanaendelea na mazungumzo na Arsenal kuhusu mkataba wa mkopo wa winga wa Ivory Coast Nicolas Pepe, 27. (Fabrizio Romano)
Leeds na Newcastle wanamfuatilia kiungo wa kati wa Los Angeles FC kutoka Ecuador Jose Cifuentes, 23, ambaye pia anawindwa na Brighton. (Sun)
Lazio wanatafuta kumnunua beki wa kushoto wa Tottenham Sergio Reguilon, 25. (Calciomercato – in Italian)
Nottingham Forest wana nia ya kumsajili Serge Aurier, 29. Beki huyo wa kulia wa Ivory Coast ni mchezaji huru baada ya kutolewa na Villarreal. (Footmercato, via Express)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Aston Villa wamewasilisha ofa ya mkopo kwa beki wa kati wa Poland Jan Bednarek, 26, kutoka Southampton. (Football Insider)
Wolves wamekataa dau la pauni milioni 1 kwa beki wa kati wa Ivory Coast Willy Boly, 31, kutoka Nottingham Forest. (The Athletic – subscription required)
Tottenham inaweza kumsajili Ruslan Malinovskyi wa Atalanta, 29, huku kiungo huyo wa kati wa Ukraine akiwa hana uhakika kuhusu kuhamia Marseille. (Footmercato – in French)
Nottingham Forest inamtaka beki wa kulia wa Uholanzi Hans Hateboer, 28, kutoka Atalanta. (Tutto Atalanta – in Italian)
Tottenham, Roma na Inter Milan wanavutiwa na beki wa kati wa Chelsea wa Uingereza Trevoh Chalobah, 23. (Evening Standard)