
Wizara ya afya kupitia Idara ya tiba imeendelea kutekeleza mkakati wa Wizara wa kuboresha huduma katika vituo vya kutolea huduma za afya kwa kutoa mafunzo ya huduma kwa mteja (customer service) na ubora wa huduma kwa Waganga wafawidhi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa, Wauguzi wafawidhi, Maafisa Utumishi, Wasimamizi wa ubora wa huduma, Waratibu wa huduma za tiba na Wahasibu katika Hospitali hizo.
Mafunzo hayo yameanza jana Agosti 24, Mkoani Mwanza na yanatarajia kuendelea leo na kesho kwa kundi la Waganga wafawidhi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa, Wauguzi wafawidhi, Maafisa Utumishi, Wauguzi wafawidhi, na Wahasibu katika hospitali hizo.



