Cristiano Ronaldo anaweza kuondoka Manchester United na kuelekea Napoli wiki hii. Mshambuliaji wa United wa Ureno, 37, ameanza mechi moja pekee ya Ligi Kuu msimu huu. (Metro)
Tottenham wako kwenye mazungumzo kuhusu uwezekano wa kumnunua winga wa Leeds United na Wales Daniel James, 24, kabla ya tarehe ya mwisho ya uhamisho ya Alhamisi saa 23:00 BST. (Fabrizio Romano)
Wakati huo huo, Spurs wamefufua nia yao ya kumnunua kiungo wa kati wa Atletico Madrid na Ubelgiji Yannick Carrasco, 28. (Telegraph – usajili unahitajika)
-
Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 29.08.202229 Agosti 2022
-
Je, klabu ya Barcelona ni ‘mfamaji anayetapatapa’?29 Agosti 2022
Chelsea itafuatilia usajili wa pauni milioni 70 wa beki Mfaransa wa Leicester Wesley Fofana, 21, kwa kushinikiza uhamisho wa mshambuliaji wa Barcelona wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 33. The Blues pia wanataka kumsajili winga wa Everton Mwingereza Anthony Gordon, 21, wiki hii. (Guardian)

CHANZO CHA PICHA,REUTERS
Aston Villa wana hamu kubwa ya kumnunua kocha wa Brighton Graham Potter kama mbadala wa Steven Gerrard, ambaye amepoteza mechi tatu kati ya nne za kwanza za ligi msimu huu. (Football Insider)
Newcastle wanamtaka kiungo wa kati wa Chelsea Mfaransa Tiemoue Bakayoko, 28, ambaye yuko AC Milan kwa mkopo wa miaka miwili. Nottingham Forest pia wanamwania mchezaji huyo. (Calciomercato – kwa Kiitaliano)
Crystal Palace wametoa ofa ya pauni milioni 27 kumnunua kiungo wa kati wa Chelsea na Muingereza Conor Gallagher, 22, ambaye alivutia alipokuwa kwa mkopo na The Eagles mnamo 2021-22. (Times- usajili unahitajika)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Beki wa Arsenal na Uhispania Hector Bellerin, 27, anaweza kujiunga na Real Betis, ambapo alikuwa kwa mkopo msimu uliopita. Bellerin hajaichezea The Gunners tangu Mei 2021. (Estadio Deportivo – kwa Kihispania)
Kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong, 25, atasalia katika klabu hiyo licha ya kuhusishwa pakubwa na Manchester United na Chelsea wakati wa uhamisho wa majira ya joto. (Football Espana)
Hata hivyo, De Jong anasafiri kwenda Uingereza kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili la majira ya kiangazi, na hivyo kuzua uvumi kuhusu mustakabali wake. (Mirror)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Aston Villa na Wolves zote zina nia ya kumsajili beki wa West Ham Muingereza Craig Dawson, 32. (Sun)
Juventus watajaribu kumsajili kiungo wa kati wa Aston Villa na Brazil Douglas Luiz, 24, wakishindwa kufikia makubaliano na Paris St-Germain kumhusu Leandro Paredes, 28 wa Argentina. (Sky Sport Italia – kwa Kiitaliano).
Beki wa Liverpool na Uholanzi walio chini ya umri wa miaka 21 Sepp van den Berg, 20, anatazamiwa kujiunga na Schalke kwa mkopo. (The Athletic-Usajili unahitajika)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Leicester City wanafanya mazungumzo na Schalke kuhussu usajili wa kiungo wa kati wa Morocco Amine Harit, 25. (Sky Sports)
Fulham wamefikia mkataba na Paris St-Germain kumsajili beki wa Ufaransa Layvin Kurzawa, 29, wakati The Cottagers pia wanafanya juhudi za kumnunua winga wa Roma Mholanzi Justin Kluivert, 23. (Mail)