
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Bora na Serikali za mitaa imepokea na kujadili taarifa kuhusu Utekelezaji wa Programu ya Lipa kutokana na Matokeo (Education Performance for Result-EP4R), Mradi wa Kuimarisha Ujifunzaji katika Elimu ya Awali na Msingi – BOOST na Mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (Secondary Education Quality Improvement Project-SEQUIP) tarehe 30 Agosti 2022
Miradi hiyo inatekelezwa chini ya Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kushirikiana Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa lengo la kuinua ubora wa elimu ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya elimu katika Shule za Msingi na Sekondari.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa iliongozwa na Mhe. Jaffari A. Chaurembo, Mbunge wa Jimbo la Mbagala, Makamu Mwenyekiti Mhe. Denis L. Londo, Mbunge wa Jimbo la Mikumi na kuhudhuliwa na wajumbe wa kamati hiyo.
Aidha, Kamati iliudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa, Naibu Waziri Mhe. David Silinde, Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt. Charles Msonde na Wakurugunzi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI.




