Everton na Leeds wameungana na Southampton kujaribu kumsajili Cody Gakpo. PSV Eindhoven ilikataa ombi la euro 25m (£21.4m) kutoka kwa Saints mapema wiki hii kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 23. (Telegraph – subscription required)
Brighton wanasema hawatashinikizwa kumuuza kiungo wao wa kimataifa wa Ecuador Moises Caicedo, 20, ambaye amekuwa akihusishwa na uhamisho wa £42m kwenda Liverpool. (TalkSport)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Chelsea wako kwenye mazungumzo ya kukamilisha dili la £77m kwa mlinzi wa Croatia Josko Gvardiol, 20, kufikia tarehe ya mwisho ya uhamisho wa Alhamisi, kwa nia ya kumrudisha kwa mkopo katika klabu yake ya sasa ya RB Leipzig. (Mail)
Manchester United itamruhusu Aaron Wan-Bissaka, 24, kuondoka katika klabu hiyo iwapo wataweza kukubaliana kumnunua kwa mkopo Sergino Dest wa Barcelona, 21, ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Marekani. (90min)
Arsenal na Everton ni miongoni mwa vilabu kadhaa vinavyomhitaji winga wa Shakhtar Donetsk na Ukraine Mykhaylo Mudryk, 21, na bado kuna uwezekano wa uhamisho uliocheleweshwa. (Metro)

CHANZO CHA PICHA,REUTERS
Juventus wanatazamia kukamilisha mkataba wa mkopo kumnunua kiungo wa kati wa PSG na Argentina Leandro Paredes, 28, ambaye alikuwa akivutia Arsenal. (La Gazzetta dello Sport – in Italian)
Leicester City wako kwenye mazungumzo juu ya mkataba wa pauni milioni 17.2 kumnunua beki wa Reims Wout Faes, 24, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji akionekana kama mbadala wa mlinzi wa Ufaransa Wesley Fofana, 21, ambaye anakaribia kuhamia Chelsea kwa pauni milioni 70. (Mail)
Beki wa Ivory Coast Willy Boly, 31, atafanyiwa uchunguzi wa kimatibabu huko Nottingham Forest kabla ya kununuliwa kwa pauni milioni 2.25 kutoka Wolverhampton Wanderers. (Athletic – subscription needed)
Barcelona wanaweza kumnunua beki wa kulia wa Arsenal na Uhispania Hector Bellerin, 27, ikiwa hawataweza kumpata mlinzi wa Argentina Juan Foyth, 24, kutoka Villarreal katika siku za mwisho za dirisha la usajili (90min)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Atletico Madrid wako tayari kutoa ofa ya pauni milioni 20 kumsajili kiungo wa kati wa Aston Villa na Brazil Douglas Luiz, 24, ambaye yuko katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake na Klabu hiyo ya Premier League. (Telegraph -subscription required)
Kiungo wa kati wa Valencia na Uhispania Carlos Soler, 25, anatazamiwa kujiunga na PSG kwa mkataba wenye thamani ya euro 18m pamoja na nyongeza. (Marca – in Spanish)
Kiungo wa kati wa Senegal Idrissa Gueye, 32, anatarajiwa kusafiri kwa ndege hadi Uingereza kukamilisha pendekezo lake la kuhamia Everton kutoka PSG (Athletic – subscription needed)
Klabu inayoshiriki ligi daraja la kwanza Sunderland bado ina matumaini ya kukamilisha mkataba wa mkopo wa kiungo wa kati wa PSG Mfaransa Edouard Michut mwenye umri wa miaka 19. (Chronicle)