Baada ya mchezo wa fainali ya mechi ya kirafiki ya kimataifa baina ya Simba SC Tanzania na Al Hilal ya nchini Sudani ambayo ndio iliyowalika kama wenyeji katika mchuano huyo kukamilika salama, ingawa Simba Sc ilipoteza kwa 0-1 dhidi ya wenyeeji hao katika mchezo uliochezwa hapo jana saa 2 usiku kwa muda wa saa za Tanzania, Afrika Mashariki katika uwanja wa Al Hilal Stadium, Khartoum Sudani, klabu ya Simba imekabidhi zawadi kwa uongozi wa klabu ya Al Hilal ikiwa kama sehemu ya shukrani kwa kuendeleza uhusiano mzuri kati ya kabu hizo.