Kampuni ya Masiliano Vodacom Tanzania imezindua Teknolojia ya Kasi ya Mtandao ya 5G kwa mara ya kwanza hapa nchini, uzinduzi huo umefanyika katika jengo la JOHARI ROTANA lililopo Posta ya Zamani leo hii mapema Septemba 1,2022 ambapo mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa ni Waziri mwenye dhamana ya Mawasiliano, Habari na Teknolojia ya habari Mh. Nape Nnauye.
(@https://www.instagram.com/vodacomtanzania/)Leo tumezindua kwa mara ya kwanza mtandao wa 5G Tanzania. Tunafurahi na kujivunia kuwa wa kwanza kuleta teknolojia hii ya kipekee kwenye soko la Tanzania. Kadri teknolojia inavyoendelea kukua ulimwenguni, Vodacom itaendelea kuwekeza kwenye maendeleo ya kiteknolojia hapa nchini.
#PamojaTunaweza #YaKwanzaTanzania.