
Hospitali ya Taifa Muhimbili imesaini mkataba na Kampuni ya Medel kutoka nchini Austria wenye lengo la kuanzisha maabara ya kwanza ya aina yake Afrika Mashariki ili kufundisha na kuboresha upasuaji wa sikio kwa wataalamu wa ndani na nje ya nchi.
Akisaini mkataba huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru ameshukuru kwa ushirikiano huo ambao unalenga kukuza taalamu sambamba na kwenda na kasi ya ukuaji wa sayansi na teknolojia.
“Tunashukuru Kampuni ya Medel kwa kushirikiana na Muhimbili kwa kuanzisha maabara hii ambayo itaenda kusaidia wataalamu wetu wa ndani na wa nchi jirani kuja kupata elimu kwetu na pia kupata madaktari bingwa wengi”, amesema Prof. Museru
Kwa upande wake, Bw. Fayaz Jaffer ambaye ni Mtaalamu wa kupima masikio, amesema maabara hiyo ya kisasa ambayo itasadia kutoa mafunzo kwa wataalamu, pia itapunguza madaktari bingwa hawa kwenda kupata mafunzo haya nje ya nchi na vilevile itasaidia kuleta wataalamu wengine kutoka hospitali za rufaa kuja kufanya mafunzo hayo hapa.
“Medel kwa kushirikiana na Muhimbili inatengemea kuwaleta madaktari bingwa kutoka nchi za jirani kuja kufanya mafunzo hapa kwani watu wengi watapata huu ujuzi na pia itasaidia kwa wanafunzi ambao wataingia kwenye fani hii kupata ujuzi zaidi”, amesema Bw. Jaffer
Reposted from @muhimbili_taifa