
Kocha Denis Lavagne (kulia) ni raia wa Ufaransa, mwenye wasifu mkubwa, akiwa na leseni ya juu ya ukocha (UEFA Pro Licence), amekuja katika klabu ya Azam kuchukua nafasi kocha wa zamani alioondoka Abdihamid Moallin.
Lavagne anatarajiwa kuwasili hapa nchini siku ya leo Jumanne kwani ameripotiwa kuwa yupo Qatar na wakala wake kuja Tanzania, tayari kuanza rasmi majukumu yake ndani ya klabu hio.
Mfaransa huyo wake ni kocha wa viwango vya juu sana akiwa na uzoefu na soka la Afrika, amewahi kufundisha timu ya Taifa ya Cameroon (2011-2012), miamba ya Algeria, USM Alger na JS Kabylie.
Aidha amewahi kufundisha vigogo wa Tunisia, Etoile Du Sahel (2013), Smouha ya Misri, Coton Sports (Cameroon), Al Hilal ya Sudan.
Moja ya mafanikio yake ni kufika fainali ya michuano ya Lugi ya Mabingwa Afrika mwaka 2008 akiwa na Coton Sport ya Cameroon na kupoteza dhidi ya Al Ahly ya Misri kwa jumla ya mabao 4-2.
Ubora wa mbinu zake, zilimwezesha mwaka jana, kuiongoza JS Kabylie ya Algeria kushika nafasi ya pili kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, ikicheza fainali na Raja Casablanca ya Morocco na kupoteza kwa mabao 2-1.
Mtaalamu huyo ni kocha wa makombe, kwani aliiwezesha Coton Sport kutwaa mataji manne ya ligi (2007, 2008, 2010, 2011), aliiongoza Al Hilal kutwaa taji la ligi mwaka 2016, aliiongoza JS Kabylie kubeba taji la Kombe la FA (2021) na Etoile Du Sahel kutwaa ubingwa kama huo Tunisia mwaka 2013.