Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan, leo amesaini kitabu cha maombolezo kufuatia Kifo cha Malkia Elizabeth II (96) wa Uingereza, Â aliyeaga dunia jana nchini Uskochi.
Rais Samia amesaini Kitabu hicho katika makazi ya Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Oysterbay jijini Dar es Salaam.