Baada ya mahakama kutoa uthibitisho juu ya ushindi wa William Ruto katika uchaguzi mkuu Kenya nafasi ya Urais, hii leo Ruto anaapishwa na kuanza kuhudumu katika nafasi hio akimpokea kijiti Rais Uhuru Kenyatta ambaye ndie anaachilia nafasi.
1966:William Samoei Kipchirchir Ruto alizaliwa mnamo Desemba 21 huko Sugoi, Uasin Gishu, na Daniel na Sarah Cheruiyot. Baadaye alijiunga na Shule ya Msingi ya Kerotet kabla ya kuendelea hadi Shule ya Sekondari ya na Shule ya Upili ya Wavulana ya Kapsabet
1991: Alimuoa Rachel Chebet na wanaishi Dagoretti, Nairobi. RaisDaniel Moi wakati huu alikutana na Ruto, mkutano ambao ulibadilisha misha yake.
1997: Anawania kiti cha ubunge na kuchaguliwa kuwa mbunge wa Eldoret Kaskazini, akimshinda aliye madarakani na mwenyekiti wa tawi la Uasin Gishu wa chama cha Kanu na waziri msaidizi Reuben Chesire, mshirika wa Moi. Baadaye aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa uchaguzi wa Kanu.
2012: Mahakama ya ICC mnamo Januari ilitangaza kwamba washukiwa wanne kati ya sita, akiwemo Ruto, Sang, Kenyatta na Francis Muthaura watakabiliwa na kesi ya kutenda uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2007
2013: Alichaguliwa Naibu Rais na kuapishwa Aprili 9 baada ya Jubilee kuishinda Cord katika uchaguzi wa Machi 2013, na kupata asilimia 50.07 dhidi ya asilimia 43.31 ya Bw Odinga. Ushindi unapingwa katika Mahakama ya Juu lakini ushindi huo unaidhinishwa.
2016: Kesi yake katika mahakama ya ICC yaporomoka mwezi wa Aprili, huku mahakama ikiamua kuwa hakuna ushahidi wa kutosha baada ya mashahidi muhimu kujiondoa. Mnamo Septemba, wakiwa na Kenyatta, wanabadilisha muungano wa Jubilee kuwa Jubilee Party kabla ya uchaguzi wa 2017. Alikuwa mgombea mwenza wa Kenyatta.
2017: Wakiwa na Rais Uhuru, walitangazwa washindi katika uchaguzi wa Agosti baada ya kupata asilimia 54 ya kura dhidi ya Nasa, inayoongozwa na Bw Odinga na mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka. Mahakama ya Juu, hata hivyo, ilibatilisha uchaguzi huo na kuagiza uchaguzi mpya mwezi Oktoba. Nasa ilisusia uchaguzi mpya na wanatangazwa washindi kwa asilimia 98 ya kura zote zilizopigwa. Wanaapishwa mnamo Novemba 28, 2017.
2020: Mnamo Desemba, Chama cha Party of Development and Reforms kilibadilisha rasmi jina lake hadi United Democratic Alliance (UDA) na hatua hiyo inasemekana kupata baraka za Dkt Ruto kama chombo chake cha kisiasa cha 2022.
2021: Ajiunga rasmi na UDA na kuachana na bosi wake,Kenyatta kisiasa .
2022: Atangaza kuwa atagombea urais kwa tiketi ya UDA chini ya Muungano wa Kenya Kwanza.
Agosti 15, 2022: Atangazwa kuwa Rais Mteule na mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati baada ya kupata 7,176,141, ikiwa ni asilimia 50.49 ya kura zilizopigwa, dhidi ya mgombea urais wa Azimio Odinga 6,942,930 au asilimia 48.85.
Septemba 5, 2022: Mahakama ya Juu zaidi yathibitisha kwa kauli moja ushindi wake baada ya Bw Odinga na mgombea mwenza wake, Bi Martha Karua, kupinga matokeo ya uchaguzi.
Main Source: BBCSWAHILI