
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula, jana Septemba 15, 2022 amekutana na kuzungumza na Wataalam kutoka Wizara za Maendeleo ya Jamii, Wizara ya Afya pamoja na Ofisi ya Rais-TAMISEMI smabamba na Wadau wa D-TREE kwenye kikao chenye lengo la kutambulisha Mradi wa JAMII NI AFYA unaotekelezwa na Shirika la D-TREE.
Dkt. Chaula akifungua kikao hicho kilicholenga kujadili utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) amesema katika utekelezaji wa Mradi huo wadau wanatakiwa kuunganisha mradi huo na Sayansi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto kwenye huduma zinazotolewa na Wahudumu wa Afya.
Dkt Chaula amewaasa watekelezaji wa miradi inayoanzishwa kuhakikisha inaendana na Miradi ambayo tayari imeanzishwa huko nyuma kuliko kuanza upya ili kuwa na matumizi mazuri ya rasilimali zilizopo.



