Beki wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 21 William Saliba amedokeza kuwa atasaini mkataba mpya na Arsenal ikiwa klabu hiyo itampa masharti mapya. (Sky Sports)
Juventus walikuwa wanatazamia kumteua Roberto de Zerbi iwapo watamtimua Max Allegri, na walitaka kuteka nyara uhamisho wa Brighton kwa meneja huyo wa Italia. (Times – subscription required)
Real Madrid wamepunguza nia yao ya kumnunua fowadi wa Ufaransa Kylian Mbappe, 23, na hawatamfuatilia tena nyota huyo wa PSG ikiwa hana nia ya kusajiliwa na timu hiyo (Marca – in Spanish)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Thomas Frank anasema “anafuraha sana” kusalia katika klabu ya Brentford baada ya kuhusishwa na kazi ya mkufunzi wa Leicester. (Sky Sports)
Chelsea wanajiandaa kumteua Christoph Freund kama mkurugenzi wao mpya wa michezo baada ya kukubaliana na Red Bull Salzburg. (Fabrizio Romano)
Celtic wanavutiwa na mshambuliaji wa klabu ya Maccabi Tel Aviv na Israel miongoni mwa wachezaji walio na chini ya umri wa miaka 21 Oscar Gloukh, 18, na wanaweza kutuma ofa ya pauni milioni 8 mwezi Januari. (Record)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Winga wa Chelsea na England Callum Hudson-Odoi, 21, anasema kuwa ameambiwa na mmiliki wa klabu hiyo Todd Boehly bado ana mustakabali Stamford Bridge, licha ya kutumwa kwa mkopo Bayer Leverkusen. (Mail)
Mchezaji anayelengwa na Manchester United Cody Gakpo, 23, amevumilia mwanzo “mgumu” wa msimu baada ya winga huyo wa Uholanzi kuhusishwa na kuondoka katika klabu hiyo, anadai mkurugenzi wa michezo wa PSV Marcel Brands. (ED – in Dutch)
Mchezaji anayelengwa na klabu ya West Ham Dan-Axel Zagadou, 23, anatarajiwa kujiunga na Stuttgart baada ya beki huyo wa Ufaransa kuondoka Borussia Dortmund majira ya joto. (Kicker – in German)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Sean Dyche na Nathan Jones ni miongoni mwa waliopendekezwa mapema kuwa meneja wa Cardiff baada ya Steve Morison kutimuliwa siku ya Jumapili (Wales Online)
source; BBC SWAHILI.COM