Kampuni ya Mawasiliano Tigo Tanzania imeleta MCHONGO MPYA #2 kupitia kampeni yao ya WAKISHUA WA TIGO, ufahamikao kama “Wakishua Twenzetu Qatar na Hisense” ikiwa ni muendelezo wa utoajiwa fursa kwa wateja wake katika mfumo wa Kidigitali, hapo awali ilikuwa ni mchongo wa Kusikiliza Burudani ya Muziki kupitia Boomplay: Yaani hii ni kwa mara ya kwanza Tigo kushirikiana na Hisense mshirika rasmi wa kombe la dunia yazindua promosheni ya Wakishua Twenzetu Qatar na Hisense ambapo wateja wa Tigo Pesa watapata fursa ya kujishindia tiketi ya kwenda Qatar kushuhudia kombe la dunia, zawadi za vifaa vya nyumbani vya Hisense pamoja na bonus za papo hapo za dakika na SMS.
Kampuni hio inaeleza kuwa “Zitatolewa tiketi 50 za kwenda kutazama mechi ya kandanda mubashara nchini Qatar au vifaa vya nyumbani vya Hisense (TV ya kisasa, sound bar, jokofu/friji na microwave).” Mr Jason Xu-@hisense.tz Key Account Manager for Tanzania Exports
“Ili kuingia kwenye droo mteja anatakiwa kufanya miamala ya Tigo Pesa kama vile malipo ya bidhaa na huduma kupitia Lipa kwa Simu, Kulipa bili, Malipo ya Serikali, kutuma pesa (Tigo-Tigo), Kuweka pesa, kutoa pesa benki, kununua muda wa maongezi na vifurushi pamoja na kupokea pesa kutoka nje ya nchi.” Angelica Pesha-Afisa Mkuu wa Tigo Pesa.
“Hii ni fulsa kwa watazania wote kutumia fulsa hii iliyotolewa na mshua pamoja na @hisense.tz ili uweze kwenda kushuhudia mechi za kombe la dunia, Fanya miamala na Tigo Pesa na twenzetu Qatar na Hisense.’ Feisal Salum (@feisal194 ) -Balozi Wakishua
“Mchongo wa Mshua uko wazi sasa tukifanya miamala tunakwenda Qatar unakosaje nafasi hii fanya chochote na Tigo Pesa na Tukutane Qatar”