Nchi ya Tanzania imechaguliwa kuwa miongoni wa wajumbe wa Baraza Kuu la Shirika la Mawasiliano Duniani ITU kwa kura 141 kati ya 180 zilizopigwa kwenye uchaguzi uliofanyika katika Mkutano Mkuu wa Shirika hilo (ITU PP22) jijini Bucharest, nchini Romania, Tarehe 3 Octoba, 2022
Kuchaguliwa kwa Tanzania kuwa Mjumbe wa Baraza la ITU kunaipa Nchi nafasi muhimu kutetea masuala yanayohusu ukuzaji wa teknolojia ya Mawasiliano na namna zinavyowezesha upatikanaji wa Huduma mbalimbali na kuboresha Maisha ya wananchi kila siku.
Tanzania inaungana na Nchi Wanachama 13 wa ITU kuwakilisha kanda D kuwa Wajumbe wa Baraza hilo kwa kipindi cha miaka Minne kuanzia 2023 hadi 2026.