Kitendo cha nyota wa Ghana anayekipiga mnamo klabu ya Simba SC, Augustine Okrah kuvua jezi yake akiwa anashangilia kwa furaha isio na mfano baada ya kutikisa nyavu ya goli la mpinzani wao Yanga na kubadilisha Scoring Board kusomeka 1-0 ndani ya dakika 15′ za kipindi cha kwanza Derby ya Kariakoo kabla ya Yanga kulejesha goli Dakika ndani ya nyongeza 45’+2 ambalo lililosalia kufanya sare ya 1-1, ilipelekea Simba kuadhibiwa kupitia mchezaji huyo kwa kupata kadi ya kwanza ya njano kwa utovu wa nidhamu, ikijumuisha madhambi mengine katika soka yaliosababisha kadi nne nyingine kutoka kwa wachezaji wengine wa klbu hio kama vile kadi ya njano iliyoelekezwa kwa Cletous Chama na Mohammed Hussein, Habib Kyombo na Mzamiru Yasin kufanya zifike tano dhidi ya Nne kwa madhambi yaliofanyika na klabu ya Yanga.
Kulingana na Tafsiri wa Sheria 17 za mchezo wa mpira wa miguu zilizopititwa kutumika kimataifa na FIFA, kiwango hicho cha makosa yaliojitokeza mara tano inajidhihirisha ni kiwango cha juu cha utovu wa nidhamu ulio katika klabu hivyo kuna jambo kubwa linatakiwa lifanyike kujinasua katika hilo kama uongozi wa klabu kiujumla.