Benki ya CRDB yashiriki katika Kongamano la sita la TEHAMA (TAIC) lililofanyika visiwani Zanzibar linalofanyika kuanzia tarehe 26 hadi 28 Novemba 2022.
Kongamano hilo limezinduliwa na Rais wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, na taasisi kutoka ndani na nje ya nchi.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi Mkurugenzi Mtendaji Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alibainisha kuwa kwa kushirikiana na Tume ya TEHAMA, katika kongamano hilo Benki ya CRDB inakwenda kuzindua programu wezeshi kwa wajasiriamali vijana na wanawake wenye biashara na mawazo bunifu katika sekta mbalimbali ikiwamo TEHAMA iliyopewa jina la “IMBEJU”.
Kauli mbiu ya Kongamano la TAIC mwaka huu ni “Mabadiliko ya Kidijitali kwenye Uchumi wa Buluu kwa Maendeleo ya Jamii na Kiuchumi”


