Benki ya NMB yatambulishwa rasmi kuwa Benki ya Kwanza Afrika kutunukiwa cheti cha Edge kinachoitambua kama muajiri anayezingatia masuala ya usawa wa kijinsia mahala pa kazi.
Huu ni ushahidi tosha wa jitihada zake za kujenga usawa wa kijinsia ndani ya benki hio na katika jamii inayoizunguka kupitia huduma zake za kifedha.
Imepokea cheti hicho kutoka kwa taasisi ya The EDGE Certified Foundation yenye makao makuu yake Zug, Uswisi.
Cheti hiki kimepokelewa na Afisa Mkuu wa Rasilimali Watu Benki ya NMB – Bw. Emmanuel Akonaay kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la IFC Tanzania na Burundi – Frank Ajilore aliyeambatana na Mkuu wa Masuala ya Kijinsia Afrika – Anne Kabugi.
Wengine waliohudhuria hafla ya makabidhiano ni Afisa Mkuu wa Huduma Shirikishi Benki ya NMB- Bi. Nenyuata Mejooli, Afisa Mkuu wa Udhibiti – Bi. Doreen Joseph na viongozi wengine wa benki hio.
Imewashukuru wafanyakazi, wateja pamoja na wadau wake kwa kuwa sehemu kubwa ya hatua hii.


