Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ametoa wito kwa wazazi wenye watoto walemavu kutowaficha bali wawatoe wapate elimu ili waweze kuonesha vipaji vyao.
Dkt. Gwajima ameyasema hayo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika mashindano ya Dunia ya urembo, utanashati na mitindo kwa watu wenye ulemavu wa kusikia(viziwi) yaliyofanyika tar 29 Oktoba, 2022 Jijini Dar es salaam.
Dkt. Gwajima amempongeza Rais Samia kwa kutoa kipaumbele kwenye michezo na kusisitiza kuwa mashindano hayo yanasaidia kuleta upendo mshikamano na umoja wa mataifa mbalimbali.
Mrembo kutoka Tanzania Khadija Kinyama ameibuka mshindi katika mashindano hayo huku Australia ikishika nafasi ya kwanza kwenye upande wa watanashati.

