kocha mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amefunguka kuhusu hali ya kikosi cha klabu hio kuelekea mchezo wao wa Novemba 2,2022 dhidi ya CLUB AFRICAIN kutokea chini Tunisia “Wachezaji wako tayari na wameahidi kupambana, tunaomba sapoti kwa Mashabiki wetu kujitokeza kwa wingi, nguvu yao ni muhimu sana kwenye mchezo wetu wa kesho” Kocha mkuu Nabi

“Tunajua umuhimu wa mchezo huu Kwetu kwa Mashabiki na kwa Watanzania wote kwa ujumla na matarajio yetu ni kuhakikisha tunautumia Uwanja wa nyumbani kupata matokeo mazuri” Kocha Mkuu Nasreddine Nabi
Club Africain wana timu nzuri na Wachezaji wenye uzoefu pamoja na Wachezaji chipukizi. Ni wazuri kwenye mipira ya kufa na mashambulizi ya haraka, pamoja na kwamba tunahitaji matokeo mazuri nyumbani pia tutacheza kwa tahadhari tusiruhusu goli” Kocha Mkuu Nabi