
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. David Sillinde amesema ujenzi wa matundu ya vyoo unazingatia mahitaji ya wanafunzi wote wakiwemo wavulana na wasichana pamoja na wanafunzi wenye maitaji maalumu.
Silinde ameyasema hayo jana Novemba 8, 2022 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mhe. Samtiely Kilumba Mbuge wa Viti Maalumu aliyetaka kujua kama kuna haja ya Serikali kujenga vyoo maalumu kwa ajili ya wanafunzi wa kike katika madarasa mapya yanayojengwa hivi sasa.
Amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI itaendelea kuzisimamia na kuzielekeza Mamlaka za Serikali za Mitaa pindi wanapo jenga shule mpya wazingatie kujenga matundu ya vyoo kulingana na michoro na ramani zote zinazotumwa kwao kwa kuwa ndani ya michoro hiyo imejumuisha chumba maalumu cha wasichana kwa ajili ya kijisitiri wanapokuwa katika siku zao (hedhi) lengo likiwa ni kuhakikisha watoto hao hawakosi masomo pindi wakiwa kwenye hedhi ili kuweza kuwasaidia.
