Kwa mujibu wa Afisa Mkuu wa Teknolojia wa kombe la Dunia 2022 chini ya FIFA, Niyas Abdulrahiman, ameeleza kuwa matukio yote yatafuatiliwa na kurekodiwa na kamera zenye teknolojia ya utambuzi wa sura ambazo zitatumika kutoa mrejesho wa taarifa ya mtu kwa kutambua sura yake.
Jumla ya kamera elfu 15 zenye teknolojia ya utambuzi wa sura zitatumika katika viwanja nane vitakavyotumika kwaaili ya michuano ya kombe la Dunia 2022 nchini Qatar ambayo itaanza rasmi tarehe 20 mwezi huu.
Kamera hizo zitakuwa zikiwafuatilia wachezaji na watu mbalimbali watakaoingia ndani ya viwanja hivyo.
Teknolojia hiyo itaendeshwa na Kituo cha Udhibiti na Ufuatiliaji cha ASPIRE ambacho ndicho chenye dhamana ya kusimamia viwanja vyote nane.
Maeneo mengine yatakayozingatiwa na kupewa kipaumbele ni vituo vya treni na mabasi.