Benki ya NMB ikisalia kuwa mshirika mkubwa wa maendeleo nchini, imepokea tuzo tatu kubwa kutoka kwa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) zinazoitambua benki hio kama mlipa Kodi Mkubwa nchini kwa mwaka 2021/2022.
Tuzo hizo ni:



Tuzo hizi ni matokeo ya kuzingatia kanuni bora za ulipaji kodi, ufanisi katika kujiendesha na ubunifu wa suluhishi bora za kifedha zenye manufaa kwa wateja wake.
Tuzo hizo zimepokelewa na Afisa Mtendaji Mkuu wetu, Bi. Ruth Zaipuna kutoka kwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia, Mhe. Nape Nnauye wakati wa hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Bi. Ruth aliambatana na Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB, Juma Kimori na wafanyakazi wengine wa Benki.
Ikiwa ni mdau wa maendeleo, imeahidi kuendelea kuendesha biashara zake kwa kuzingatia sheria na kanuni za nchi ili kuchangia kikamilifu ujenzi wa uchumi wa Taifa.