
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Angellah Kairuki amemuagiza katibu Mkuu Ofisiya Rais –TAMISEMI Prof.Riziki Shemdoe kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya kuongeza madarasa katika shule ya Msingi ya Mpandamlowoka iliyopo katika kijiji cha Mpandamloweka, Kata ya Igwisi Halmashauri ya Wilaya Kaliua Mkoani Tabora.
Ametoa agizo hilo Novemba 20, 2022 wakati akikagua ujenzi wa madarasa manne katika shule ya Sekondari Isike, ikiwa ni maandalizi ya kuwapokea wanafunzi watakaojiunga na kidato cha kwanza Januari, 2023, Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, Mkoani Tabora.
Akijibu hoja ya Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Mhe.Paul Chacha aliyeeleza uwepo wa darasa lenye mikondo 45 lililopo katika Kijiji cha Mpandamlowoka,kata ya Igwisi, Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Waziri Kailuki amesema Serikali kupitia mradi wa kuimarisha ujifunzaji katika elimu ya awali na msingi (Boost) itaongeza madarasa hayo kwa lengo la kupunguza msongamano kwa watoto.
Amemtaka Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais –TAMISEMI kuhakikisha wanafuatilia na kufanya tathmini katika shule hiyo ya msingi ili kupata hali halisi ya uhitaji wa madarasa katika kata hiyo.
Waziri Kairuki amesema kuwa Kijiji cha Mpandamlowoka kinauhitaji mkubwa wa madarasa kwa kuwa na wanafunzi zaidi ya 2000 jambo ambalo linaongeza msongamano wakati Serikali imejikita katika kuhakikisha inajenga miundombinu ya madarasa ili kupunguza msongamano kwa watoto na kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.
Aidha kwa upande wa ujenzi wa miundombinu ya barabara katika Kijiji hicho Waziri Kairuki ametoa siku 14 kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa barabara za Mijini na Vijijini TARURA Mhandisi Victor Seif kuhakikisha anafika katika kijiji hicho kwa ajili ya kutatua changamoto ya barabara

