Ripoti zinamhusisha Gwiji wa soka wa zamani wa nchini England, David Beckham kuwa yuko tayari kuwania ununuzi wa klabu ya Man United baada ya wamiliki wake wa muda mrefu familia ya Glazers kuamua kuiweka sokoni.
Anatafuta nafasi ya kufanya mazungumzo na wengine ili kuungana katika kuinunua Klabu hio. Kwa uwezo wake binafsi, Gwiji huyo hatoweza kufanya ununuzi wa klabu hiyo.
Hata hivyo wanunuzi kadhaa wanaweza wakapendelea kuungana naye ili kuongeza nguvu katika mbio hizo za kuinunua United.
Beckham amewahi kukipiga nmano klabu hiyo kwa miaka mingi hapo awali, ndio maana historia yake muhimu kwenye michuano ya soka la England na dunia, inafanya kuwa uwepo wake kwenye muungano wa wawekezaji watakaojitokeza utakuwa wenye thamani ya juu na wa kipekee.
#KocnceptSports
