Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB,Bi. Ruth Zaipuna, akimkabidhi Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya NMB, Bw.Benson Mahenya moja ya tuzo 18 za kitaifa na kimataifa katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya NMB, Bw. Ramadhan Mwikalu na kulia ni Afisa Mkuu Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Bw.Filbert Mponzi. Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi NMB wakiwa na Menejimenti ya NMB, katika picha ya pamoja wakiwa na baadhi ya tuzo ilizoshinda benki hiyo, baada ya kuzitangaza kwenye hafla iliyofanyika Makao Makuu ya NMB.: Baadhi ya Tuzo kati ya 18 za kitaifa na kimataifa ilizotunukiwa Benki ya NMB.