Aliyekuwa Kocha Mkuu Simba SC, Franco Pablo Martin amekanusha kuhusu kupata mwaliko kutoka Klabu ya Simba SC kwaajili ya kufanya mazungumzo ya kumrejesha kocha huyo katika Benchi la Ufundi la Klabu hiyo.
Ikiwa Simba SC inaendelea na Mchakato wa Kumsaka Kocha Mkuu Mpya atakayefanya kazi na Kocha Juma Mgunda, ambaye kwa sasa anakaimu nafasi ya Kocha Mkuu, baada ya kuondoka kwa Kocha Zoran Maki tangu mwezi Septemba.
Kocha Pablo ameonekana akiwa jijini Dar es salaam tangu mwishoni mwa juma lililopita na hapo jana Jumapili ya Novemba 27,2022 alikuwa Azam Complex-Chamazi akifuatilia mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kati ya Azam FC dhidi ya Coastal Union.
Baada ya kupewa nafasi ya kueleza ni nini haswa kilichojili juu ya ujio wake hapa chini, Kocha huyo kutoka nchini Hispania akafuguka kuwa amekuja nchini kwa mambo yake Binafsi na hana mwaliko wa aina yeyote kuhusiana na Klabu hio, inayotajwa kuwa kwenye mpango wa kumrudisha kazini.
“Nipo hapa kiwa mambo yangu binfasi, sina mwaliko wowote na Simba SC, siwezi kukwambia naondoka lini.” alisema Kocha Pablo
Simba SC iliachana na Kocha Pablo Machi 31 mwaka huu baada ya kushindwa kuivusha klabu hiyo kwenye hatua ya Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara, akifungwa na mtani wake wa jadi Young Africans kwa goli 1-0.