
Benki ya KCB Tanzania imeshiriki kikamulifu kongamano la wanawake la ‘Sneakers and Heels’ ambalo kwa mwaka huu limeangazia zaidi wanawake wanao jishughulisha na Sekta ya Utalii.
Kongamano hili ni kiunganishi cha wanawake na shabaha yake ni kuwakutanisha wanawake pamoja na kuendesha mjadala wenye kutafuta suluhu ya changamoto mbalimbali zinazo wakumba wanawake zikiwemo zile za kiuchumi.
Benki ya KCB Tanzania inaamini katika kuwezesha wanawake na hii ni kutokana na mchango wao mkubwa katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo katika nyanja tofauti.