Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima auzindua mpango mkakati wa sekta binafsi katika kutekeleza masuala ya chakula na lishe, wakati alipomwakilisha Waziri Mkuu mhe. Kassim Majaliwa katika mkutano mkuu wa 8 wa mwaka wa masuala ya chakula na lishe, uliofanyika mkoani Mara Disemba 06, 2022

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza katika uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Lishe.
NUKUU ZA MHE. KASSIM MAJALIWA MAJALIWA (MB.), WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA NANE WA WADAU WA LISHE
06 DESEMBA 2022, MARA ALIPO WAKILISHWA NA DKT. DOROTHY GWAJIMA
“OR-TAMISEMI ihakikishe Mikataba ya Lishe kati ya Mheshimiwa Rais na Wakuu wa Mikoa inaendelea kuboreshwa kwa kuingiza viashiria vitakavyosaidia kuongeza uwajibikaji wa sekta nyingine na kutoa taarifa.
“OR – TAMISEMI iendelee kusimamia Sekretarieti za Mikoa na Serikali za Mitaa kuhakikisha zinatenga kiasi cha shilingi 1,000 kwa kila mtoto mwenye umri chini ya miaka mitano na kuhakikisha fedha hizo zinatolewa kwa wakati na kutumika kwa malengo kusudiwa. “
“Mikoa na Halmashauri zitumie vizuri Mwongozo wa Kitaifa wa Utoaji wa Huduma ya Chakula na Lishe kwa Wanafunzi wa Elimu ya Msingi na kuhakikisha utekelezaji wa mpango huo unajumishwa ndani ya mipango na bajeti kila mwaka na afua zilizoainishwa zitengewa fedha za kutosha”
“Sekta binafsi ziongeze kasi ya uwekezaji wa uzalishaji wa vyakula vilivyorutubishwa pamoja na kuwekeza katika kuzalisha virutubishi nchini ili kupunguza gharama kubwa ya uagizaji wa virutubishi hivyo kutoka nje ya nchi.
“Taasisi za elimu ya juu ziendelee na tafiti za masuala ya lishe pamoja na kuhakikisha zinatumila kuboresha sera na mikakati yetu kwa kuelekeza afua bora zaidi za kimkakati za kupambana na utapiamlo”
“Watendaji wakuu wote katika Wizara husika, Idara, Wakala na Taasisi za Serikali ziendelee kufanya tathmini za utekelezaji wa Mpango wa Pili Jumuishi wa Kitaifa wa Masuala ya Lishe hususan afua zilizoainishwa katika mpango”
“Wadau wa maendeleo hakikisheni miradi inayoandaliwa inagusa wananchi moja kwa moja na kuhakikisha uwekezaji unafanyika kwenye Mikoa yenye changamoto kubwa ya lishe pamoja na ile yenye wadau wachache ili kupanua wigo wa utoaji wa huduma za lishe na kuongezeka kwa uwiano wa watu wanaonufaika na huduma hizo”.