Timu ya Taifa ya Ureno imeweza kutinga kibabe katika nafasi ya kushiriki hatua ya Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Dunia 2022.
Imefanikisha hilo baada ya kuipa kichapo kikali Timu ya Taifa ya Uswizi (Switzerland) kwa jumla ya mabao 6-1 katika mchezo uliochezwa Disemba 06,2022 huko nchini Qatar.
Kiwango cha Timu hio kilikuwa maradufu ya wapinzani wake, kwani waliweza peleka mashambulizi mengi ambayo baadhi yake hayakuweza tu kufanikisha kuleta magoli mengine zaidi.