
Benki ya CRDB ikiwa katika muendelezo wa kuboresha na kutoa huduma bora kwa wateja imeleta njia nyingine mbadala ya kutuma maoni kwa SMS, sasa unaweza kutupatia maoni yako muda wowote kwa kututumia Ujumbe mfupi wa maneno kwenda namba 15089 Bure.
Hafla ya uzinduzi wa huduma hii kwa kanda ya nyanda za juu iliongozwa na mgeni rasmi Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya Bi. Leah Gawaza ikihudhuriwa na Mkuu wa kitengo cha Huduma kwa wateja, Bi. Yolanda Uriyo, Meneja wa kanda ya ziwa Bi. Jenipher Tondi, Wafanyakazi pamoja na wateja wa benki ya CRDB.

